Waziri Mkuu wa Senegal, Ousmane Sonko, amezindua sheria mpya inayoongeza maradufu adhabu ya juu kwa makosa ya mahusiano ya jinsia moja, ambapo watakaopatikana na hatia watakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela, ikilinganishwa na kifungo cha mwaka mmoja hadi mitano kilichokuwapo awali.
Muswada huo uliwasilishwa bungeni na mawaziri baada ya kuidhinishwa wiki iliyopita, hatua iliyokuja kufuatia kukamatwa kwa watu kadhaa wanaodaiwa kujihusisha na mahusiano ya jinsia moja, ambayo tayari ni kosa la jinai nchini humo.
Katika mwezi huu pekee, polisi wameripoti kukamatwa kwa wanaume 12, wakiwemo watu wawili mashuhuri na mwandishi wa habari maarufu, huku vyombo vya habari vikieleza kuwa takribani watu 30 wamekamatwa tangu operesheni hiyo ianze.
Hata hivyo, mashirika ya haki za binadamu yamekosoa hatua hiyo yakidai inaongeza ukandamizaji dhidi ya kundi la LGBTQ+.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime