BUWSSA Yaanza Matumizi ya Mita za Malipo Kabla

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) mkoani Mara imeanza kutumia mita za malipo kabla kama mkakati wa kukabiliana na changamoto ya madeni sugu ya wateja wake.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa BUWSSA, Esther Gilyoma, amesema utekelezaji huo unaendana na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kupunguza na hatimaye kuondoa malalamiko ya wananchi kuhusu ankara za maji.

Ameeleza kuwa matumizi ya mita hizo yataongeza uwazi, nidhamu ya malipo na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.

Hata hivyo katika awamu ya kwanza, BUWSSA imepokea mita 1,000 kupitia Wizara husika na wadau mbalimbali, huku zoezi la usambazaji likiendelea kulingana na upatikanaji wa rasilimali.

Sasa ili kupata undani wa  taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa moja kamili alasiri ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Evance Mlyakado tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa. 

Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii