Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imekubaliana na pingamizi lililowasilishwa na mshtakiwa Tundu Lissu kupinga taarifa ya kuongezwa kwa ushahidi (Notice of Additional Evidence) iliyotolewa na upande wa Mashtaka Februari 18, 2026.
Akisoma uamuzi huo Jaji Dustin Ndunguru, anayesimamia shauri hilo amesema kwa mujibu wa kifungu cha 308(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ushahidi unaoruhusiwa ni ule uliosahaulika kuwasilishwa wakati wa hatua ya awali ya usikilizwaji (committal proceedings) na si ushahidi mpya unaoletwa baada ya hatua hiyo kukamilika.
Aidha Mahakama imeeleza kuwa masharti ya kifungu hicho hayaruhusu kuwasilishwa kwa ushahidi mpya nje ya wigo uliowekwa kisheria, hivyo kukubaliana na hoja za utetezi.
Awali, upande wa Mashtaka uliwasilisha notisi ukitaka kuwasilisha ushahidi wa ziada kupitia kwa Amini Mahamba, ambaye ni mpelelezi wa matukio ya Oktoba 29 na baada ya tarehe hiyo, jambo lililopingwa na upande wa utetezi kwa madai kuwa halikidhi matakwa ya kisheria.
Hata hivyo kesi hiyo inaendelea katika Mahakama Kuu huku pande zote zikitarajiwa kuendelea na hatua zinazofuata kwa mujibu wa uamuzi huo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime