Zahanati ya Msasa Geita Yakamilishwa Baada ya Miaka 10 ya Kusubiri

Wananchi wa Kijiji cha Msasa, Kata ya Runzewe Mashariki wilayani Bukombe mkoani Geita, wameishukuru Ofisi ya Madini kwa kuchukua jukumu la kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho uliokuwa umekwama kwa zaidi ya miaka kumi.

Wananchi hao wametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kutembelea eneo la ujenzi, wakisema kukamilika kwa zahanati hiyo kutaboresha huduma za afya, kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika na kuongeza ustawi wa jamii kwa ujumla.

Wamesema awali walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya, hali iliyowaathiri zaidi akina mama wajawazito, watoto na wazee.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Msasa, Tulinge Paschal, amesema uamuzi wa kujenga zahanati ulitokana na changamoto kubwa za kiafya zilizokuwa zinawakabili wananchi wa eneo hilo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mgodi wa Msasa, Cosmas Bongo, amesema mgodi umeamua kukamilisha mradi huo kama sehemu ya kurudisha faida kwa jamii inayouzunguka mgodi ili wananchi wapate huduma za afya karibu na makazi yao.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii