Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Said Mtanda, ametoa siku tatu kwa Mkaguzi wa Ndani wa Mkoa huo kukagua na kutoa taarifa ya fedha Shilingi milioni 79 zilizobaki baada ya utekelezaji wa mradi wa jengo la wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe.
Mtanda ametoa agizo hilo leo Februari 10 mwaka huu wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya afya na elimu wilayani Ukerewe, akisema fedha hizo hazijaelezwa zilipo na hakuna uwazi wa matumizi yake.
Amesema haiwezekani Serikali itoe fedha halafu zisijulikane zilipotumika, huku akisisitiza kuwa uwajibikaji ni msingi wa utendaji wa viongozi na watumishi wa umma.
Mhe. Mtanda amemuonya Mkaguzi wa Ndani kuwa endapo hatatekeleza agizo hilo ndani ya siku tatu, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake, akieleza kuwa kutotekeleza maagizo ya viongozi kwa wakati ni utovu wa nidhamu kazini.
Aidha, ameamuru hatua zichukuliwe dhidi ya mtumishi wa umma aliyejipa tenda ya kusambaza kokoto kwenye ujenzi wa Hospitali ya Mkoa yenye hadhi ya Rufaa inayojengwa Ukerewe, huku yeye akiwa msimamizi wa mradi huo.
Amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia mgongano wa maslahi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili alasiri mchana ambapo msomaji wetu wa hii leo ni @Florenciapetertz tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime