Wananchi 258 Simiyu Wapata Huduma Kupitia Kliniki ya Sheria Bure

Jumla ya wananchi 258 mkoani Simiyu wamewasilisha migogoro yao ya kisheria katika Kliniki ya Sheria Bila Malipo iliyodumu kwa siku nane, iliyoendeshwa na zaidi ya mawakili 40 kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akizungumza katika viwanja vya CCM wilayani Bariadi kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Uratibu na Huduma za Kisheria Wakili Neema Ringo amesema migogoro 204 ilipokelewa na kushughulikiwa.

Amesema kati ya migogoro hiyo, 92 imepata ufumbuzi na kumalizika, huku mingine 112 ikiendelea katika hatua mbalimbali za ufuatiliaji.

Wakili Ringo amesema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu itaendelea kufuatilia migogoro hiyo hadi ipatiwe suluhu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anamringi Macha, amesema kuanzishwa kwa Kamati za Ushauri wa Kisheria kutasaidia kupunguza migogoro kwa wananchi.

Ameihakikishia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Serikali ya Mkoa wa Simiyu itaendelea kutoa ushirikiano ili Kamati za Msaada wa Kisheria ziweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa saba kamili  mchana  ambapo msomaji wetu wa hii leo ni  @Florenciapetertz tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.

Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii