Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda amepiga marufuku vitendo vyote vya kishirikina vinavyohusisha ramli chonganishi katika Mkoa wa Mwanza akisema ni uchonganishi unaovuruga amani na Serikali haiwezi kuvumilia.
Agizo hilo amelitoa akiwa wilayani Ukerewe wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Mkoa yenye hadhi ya rufaa.
Ambapo Mtanda amesema hakuna mtu atakayekubalika kuendesha shughuli za ramli chonganishi, hususan zile zinazohusishwa na kundi linalojiita ‘Kamchape’.
Amesisitiza kuwa marufuku hiyo inahusu Ukerewe na Mkoa mzima wa Mwanza, akibainisha kuwa vitendo hivyo vinahatarisha usalama na mshikamano wa jamii.
Mhe. Mtanda amesema Serikali haitavumilia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha na imani potofu zinazochochea migogoro, hofu na uhasama miongoni mwa wananchi.
Aidha amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote watakaobainika kuendelea na vitendo hivyo.
Hata hivyo amesisitiza kuwa lengo la Serikali ni kulinda amani, utulivu na maisha ya wananchi wa Mwanza.
Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa saba kamili mchana ambapo msomaji wetu wa hii leo ni @Florenciapetertz tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime