Asa Aachia Albamu Yake Akimshirikisha Wizkid
SIKU chache baada ya kuachia ngoma mbili kwa mpigo za
Mayana na Ocean, staa mrembo kutoka nchini Nigeria, Asa amezindua rasmi
albamu yake yenye ngoma kumi ndani yake, akiwashirikisha wakali kibao
akiwemo staa mkubwa wa muziki, Wizkid.
Katika albamu hiyo aliyoipa jina la V (Five), Asa pia
amewashirikisha wakali wengine kibao, akiwemo Amaarae na The Cavemen
ambapo imesheheni nyimbo zenye mahadhi tofauti, kuanzia Pop, Afrobeat na
R&B.
Akiizungumzia albamu hiyo, Asa amenukuliwa akisema
mchanganyiko wa nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo, ni uthibitisho
kwamba muziki wake umekuwa ukibadilikabadilika na kuzidi kupanga ngazi
kila kukicha kwa lengo la kukata kiu ya mashabiki wake.
Mwanadada huyo anaelezea kwamba safari hii, nyimbo zote
amezitunga akiwa jijini Lagos ambapo kuzuka kwa ugonjwa wa Corona,
kulifanya ratiba zake zote za ziara za kimuziki kusitishwa na hivyo
kumpa muda wa kutosha wa kutulia na kuandaa kazi yenye ubora wa hali wa
juu.
“Nilikuwa nyumbani nikifikiria nini cha kufanya kama
watu wengine wote walivyokuwa wakifanya kipindi cha Corona. Kwa hiyo
nikapata nafasi ya kukutana na marafiki zangu na kila mmoja kuonesha
ubunifu wake. Nilikutana na Prodyuza Priime na hakika ni mtu mzuri sana
kwenye suala la production na hapo ndipo albamu yangu ilipozaliwa.”
Anazidi kueleza kwamba mwanzo hakuwa anajua kwamba
tayari safari ya kutengeneza albamu imeanza, alidhani anaandaa nyimbo
moja moja lakini uwezo aliokuwa akiuonesha kila anapoingia studio, na
umahiri wa prodyuza Priime, ulimfanya ajikute tayari amekamilisha albamu
iliyosheheni ngoma kali tupu.
Ngoma zilizopo kwenye albamu hiyo ni hizi; Mayana, Ocean, IDG aliomshirikisha Wizkid na Nike
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii