Arteta Awaomba Mashabiki Utulivu

Arteta aliongeza kuwa mazungumzo hayo yalikuwa ya kutia moyo na yamewapa wachezaji imani mpya, akibainisha kuwa Arsenal ipo katika nafasi nzuri ya kupigania mataji manne tofauti msimu huu.

“Tumepata haki ya kuwa kwenye mashindano manne. Tutacheza kwa furaha, ujasiri na imani kwamba tutashinda,” aliongeza.

Licha ya changamoto hizo, Arsenal pia wapo njiani kufikia fainali ya Kombe la Carabao na bado wanashiriki Kombe la FA. Arteta aliwataka mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwa na imani na timu yao.

Arsenal wamekuwa wakimaliza nafasi ya pili kwa misimu mitatu mfululizo, huku wakisubiri taji la Ligi Kuu kwa zaidi ya miaka 22 sasa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii