Uwanja wa KMC Wafungiwa na TFF kwa Kukosa Vigezo

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa KMC uliopo jijini Dar es Salaam kutotumika kwa michezo ya Ligi kuu baada ya kubaini kuwa haukidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka  TFF zimeeleza kuwa  miundombinu ya uwanja huo haijakidhi matakwa ya Kanuni kama ilivyoainishwa katika masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu hali iliyopelekea kuchukuliwa kwa uamuzi huo.

Aidha kutokana na hatua hiyo klabu zote zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia viwanja mbadala kwa mujibu wa Kanuni hadi pale uwanja huo utakapofanyiwa marekebisho na kukaguliwa upya na TFF kabla ya kuruhusiwa kutumika tena.

Hata hivyo TFF imesisitiza kuwa itaendelea kusimamia utekelezaji wa Kanuni na kuzitaka klabu zote nchini kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja ili kukidhi viwango vinavyotakiwa kwa michezo ya Ligi.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii