Mitaa ya Italia Yakumbwa na Mafuriko Ghafla Kama ya Sunami – Video

Watu nchini Italia walilazimika kukimbia kuokoa maisha yao baada ya mawimbi makubwa ya bahari yanayofanana na tsunami kuvamia mitaa ya kisiwa cha Sicily ndani ya sekunde chache tu.

Katika picha za kushtua zilizonaswa  Jan 21 mwaka huu zinaonesha mawimbi makubwa yakipiga kisiwa hicho kwa nguvu, wakati dhoruba kali iitwayo Storm Harry ilipoikumba Bahari ya Mediterania ya kati.

Aidha video zilizosambazwa mitandaoni, wakazi wanaonekana wakipiga kelele na kukimbia, huku maji ya bahari yakibadilisha barabara kuwa mito yenye mkondo mkali wa maji.

Ambapo mawimbi hayo yenye nguvu yalifunika barabara na njia za waenda kwa miguu, huku povu zito la bahari likifika hadi sakafu za chini za majengo yaliyo jirani.

Baadhi ya wapita njia walilazimika kutembea ndani ya maji mengi kwa jitihada za dharura ili kufika maeneo salama.

Video nyingine inaonesha tukio la kutisha ambapo wimbi kubwa la dhoruba liligonga moja kwa moja bandari ya kisiwa cha Lipari, kilichopo karibu na pwani ya Sicily.

Ndani ya muda mfupi, maji yalifurika mitaa ya eneo hilo huku upepo mkali na mawimbi yasiyokoma yakiendelea kuishambulia fukwe.
Dhoruba ya Storm Harry ilisababisha usumbufu mkubwa katika eneo zima.

Safari za ndege na vivuko vya baharini kuelekea na kutoka Malta ziliahirishwa au kufutwa, huku vyombo vya uokoaji vya Italia vikishughulikia zaidi ya matukio 180 ya dharura.
Miji mingine ya pwani kama Málaga na Almería ilijiandaa kukumbwa na upepo mkali unaofikia kasi ya maili 43 kwa saa.

Nchini Ufaransa, maeneo ya pwani ya kaskazini-magharibi pia yalishuhudia mvua kubwa na upepo mkali, huku hali mbaya ya hewa ikiendelea kuzikumba sehemu kubwa za bara la Ulaya.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii