Marekani yaanza kuwahamisha wafungwa wa IS kutoka Syria

                         Jeshi la Marekani limesema kuwa limewahamisha wafungwa 150 wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu,                                       IS kutoka Syria na kuwapeleka Irak amapo jeshi hilo linasema mchakato huo huenda ukashuhudia wafungwa                              7,000 kuhamishwa kutoka Syria.

Hata hivyo mkuu wa vikosi vya Marekani Mashariki ya Kati Brad Cooper katika taarifa amesema kuwa amezungumza na Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa ili kuhakikisha kwamba wanajeshi wa Syria na vikosi vyengine haviutatizi mchakato huo.

Hivyo Syria juzi Jumanne ilitangaza usitishwaji wa mapigano na vikosi vya Wakurdi na kuwapatia siku nne kukubali kujiunga na serikali kuu, jambo ambalo Marekani iliwataka walikubali.

Aidha kuna zaidi ya wafungwa 10,000 wanachama wa IS na maelfu ya wanawake na watoto walio na mafungamano na kundi hilo la kigaidi katika magereza ya Syria.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii