Wakati Bunge linaanza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hasan aliwataka wabunge wasimame kuwaombea waliopoteza maisha 29 October mwaka huu.
Na kueleza kuwa kama tulivyowaahidi wananchi tutaongeza mikopo ya elimu ya juu, kwani kipindi hiki kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, tutakua na kampasi za vyuo vikuu kila mkoa.
-Dkt. Samia alisema kuwa waheshimiwa wabunge, Matarajio ya wananchi kwenu ni makubwa, matarajio yao ni kuwa mtatumia muda wenu mwingi kuwa na mijadala inayoakisi raha na karaha wanazoziona na mtasimamia na kuishauri serikali ipasavyo juu ya kutatua changamoto zao.
Aidha Dkt. Samia alifafanua jitihada za kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 128, kwa sasa muelekeo wetu ni kuendelea kupiga hatua kwenye uzalishaji wa sukari na mafuta ya kupikia, hususani uzalishaji na usindikaji wa alizeti, chikichi na ufuta.
Hata hivyo aliwataka watanzania, kujifunze kutokana na mapito yetu, hapana shaka kwamba Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia ila neno demokrasia kamili linaweza kutafsiriwa kwenye mitazamo tofauti.