Wanafunzi 52 watekwa na watu waliojihami kwa silaha Nigeria

Watu waliojihami kwa silaha wanadaiwa kuwateka nyara wanafunzi 52 katika shule moja ya kikatoliki katika jimbo la Niger nchini Nigeria.

Taarifa kutoka kwa serikali ya jimbo hilo imethibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini ikasema idadi ya wanafunzi waliotekwa bado inachunguzwa.

Taarifa hiyo imesema serikali ya jimbo la Niger, imesikitishwa na mkasa huo wa wanafunzi wa shule ya St Marys kutekwa na kuwahakikishia raia kwamba maafisa wa usalama tayari, wameanza msako wa kuwatafuta wanafunzi hao.

Hivi Karibuni Nigeriaimekuwa ikikabiliwa na visa kadhaa kama hivyo kiwemo kisa cha siku ya Jumatatu cha wanafunzi 25 wa kike kutekwa nyara katika jimbo la Kebbi.

Mashambulizi hayo yameonyesha doa lililopo katika idara za usalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi  na kusababisha rais Bola Ahmed Tinubu kuahirisha safari zake za nje ili kushughulikia tatizo hilo.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii