Uhamiaji Simiyu yaendelea na jitihada za kudhibiti Wahamiaji haramu

‎Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu inaendelea na juhudi za kuhakikisha usalama wa Taifa kwa kudhibiti wahamiaji haramu kupitia oparesheni na utoaji wa elimu kwa wadau mbalimbali wa usafirishaji.

‎‎Hayo yamezungumzwa  Novemba 20 mwaka huu katika zoezi la ukaguzi na utoaji wa elimu kwa wafanyakazi wa mabasi yanayofanya safari kati ya Mwanza, Sirari, Tarime (Nyamongo), Kahama na Runzewe, Idara ya Uhamiaji ilifanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 14 kutoka nchini Burundi — wanawake 3 na wanaume 11 — waliokuwa wakielekea nchini Kenya kwa ajili ya kazi za kulima na kazi za ndani bila vibali halali.

‎‎Zoezi hilo lilifanyika chini ya kampeni ya "Mjue Jirani Yako", inayolenga kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa Taifa kwa kutoa taarifa za wageni wasiofahamika au wanaoishi kinyume cha sheria.

‎‎Taratibu za kisheria dhidi ya wahusika zinaendelea kuchukuliwa, huku Idara ya Uhamiaji ikiendelea kutoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri kushirikiana kwa karibu na vyombo vya ulinzi na usalama ili kudhibiti wahamiaji haramu nchini.

#Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii