China imesaini makubaliano ya kufufua mradi wa TAZARA

China imesaini makubaliano ya mradi wa dola bilioni 1.4 na Zambia na Tanzania, kuboresha barabara ya reli ya TAZARA inayoyaunganisha Zambia, ambayo haina bahari na Tanzania yenye bahari ya Hindi.

Barabara hiyo ya reli iliyofadhiliwa na China miaka ya 70 kurahisisha usafirishaji wa shaba na uingizaji wa mafuta kupitia Tanzania, inabakia kuwa barabara muhimu ya kibishara  na inaonekana kutoa ushindani katika mpango wa Marekani na Ulaya wa Ukanda wa Lobito, ambayo ni njia ya reli inayounganisha Angola, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mpango huo ulisainiwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa China Li Qiang nchini Zambia, ambayo ilikuwa ziara ya kwanza ya mjumbe wa taifa hilo kwa zambia ndani ya miaka 28.  Rais Hakainde Hichilema aliusifu uwekezaji huo.

China ni miongoni mwa washirika wakubwa wa kibiashara barani Afrika na imedhamiria kutumia rasilimali asilia za bara hilo ikiwemo shaba, dhahabu, lithiamu na madini adimu ya ardhini.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii