Dkt, Samia anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi siku mbili mkoani Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Arusha kuanzia tarehe 21 hadi Novemba 22 mwaka huu.

Rais Samia anatarajiwa kuwasili leo tarehe 21 Novemba katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambako atapokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi.

Aidha kesho Novemba 22 mwaka huu, Rais Samia atahudhuria na kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuwatu nuku Kamisheni Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) itakayofanyika katika Chuo cha Kijeshi cha Monduli.

#Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii