Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hasan amesema serikali yake itaunda wizara maalumu ya vijana na itashughulikia maswala ya vijana.
Ambapo ameeleza kuwa akiwa kama Mama na mlezi wa Taifa hili ametoa maagizo kwa DPP na vyombo vya ulinzi na usalama kufuta mashtaka yote ya vijana ambao kwa namna moja au nyingine walifanya waliyoyafanya siku ya Uchaguzi kwa mkumbo na kushawishiwa. Tunahitaji tuanze upya kama taifa. -Dkt. Samia Suluhu..
Aidha kwa kuwa zaidi ya 60% ni vijana, tumeamua kama Serikali sasa kuwa na Wizara kamili ya vijana, na kuwa na washauri binafsi wa Rais katika masuala ya Vijana, ili sasa vijana watazamwe kwa namna ya upekee.
Pia tunafikiri kuanzisha madirisha maalum ya uwekezaji na uwezeshaji ya vijana (Youths Investment Windows) kama sehemu ya mikakati ya kuwaondoa vijana katika ombwe la umasikini.
Hata hivyo tunafikiria kutoa vivutio maalumu vya kikodi kwa taasisi za Umma ambazo zitatoa ajira nyingi kwa vijana kwa sababu tunafahamu, Serikali peke yake haiwezi kuajiri watu wote, ila kwa kuwezesha Sekta binafsi na kuzipa vivutio vya kikodi na kisheria basi tunaweza kupunguza tatizo la Ajira kwa vijana.
Pia tumejiwekea malengo ya kwamba hadi 2030 walau tuwe tumetenegenza mazingira ya kisheria na kibiashara yanayootosha kutengeneza wawekezaji vijana na wazawa na kutenegeza ajira za uhakika Milioni 8.
Ikiwa jitihada zozote tunazozichukua za kuleta maendeleo nchini zitalenga kuinua na kuongeza thamani ya utu wa watu wa Tanzania. Nawahakikishia kwamba, Serikali itachochea upatikanaji wa fursa za kiuchumi na kujenga matumaini kwa makundi yote mijini na vijijini.