Rais Samia Suluhu Hassan amewatakiwa kheri ya wanafunzi 595,816 wa kidato cha nne ambao wameanza mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari leo katika shule takribani 5,868 nchini.
Aidha katika ujumbe alioutoa kupitia mitandao yake ya kijamii leo Rais Samia amesema idadi hiyo ya shule inatokana na nyongeza ya shule 305 mpya, ambazo ni mara yake ya kwanza kufanya mtihani wa kidato cha nne.
Hata hivyo amesema kuwa shule hizo ni matokeo ya kazi wanayoendelea kufanya kuhakikisha kila mtoto wa Tanzania ana uhakika wa kupata elimu bora.
“Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyewaongoza tangu elimu ya awali hadi leo awajalie utulivu mwifanye na kukamilisha vyema hatua hii muhimu kwenye maisha yenu.