Nemesio Oseguera Cervantes maarufu kama El Mencho ameuawa kufuatia operesheni kubwa ya kijeshi iliyofanyika katika jimbo la Jalisco nchini Mexico.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, kiongozi huyo wa genge la Jalisco New Generation Cartel alijeruhiwa vibaya wakati wa mapambano makali kati ya wanajeshi wa serikali na wanachama wa kundi lake.
Jambo lililopelekea kufariki dunia alipokuwa akisafirishwa kwenda Mexico City kwa matibabu.
Katika operesheni hiyo, wanachama wanne wa Cartel waliuawa huku wanajeshi watatu wakijeruhiwa.
Serikali ya Marekani ilishiriki kwa kutoa taarifa za kijasusi zilizosaidia kufanikisha oparesheni hiyo.
Awali, Marekani ilikuwa imetangaza zawadi ya dola milioni 15 kwa yeyote ambaye angefanikisha kukamatwa kwa kiongozi huyo.
Aidha baada ya tukio hilo, wafuasi wa Cartel walijibu kwa kuchoma magari na kuziba barabara katika majimbo manane, hali iliyosababisha taharuki na usumbufu mkubwa wa usafiri.
Hata hivyo Mamlaka pia ziliripoti kukamatwa kwa magari ya kivita pamoja na silaha nzito wakati wa operesheni hiyo, huku hatua za kiusalama zikiendelea kuimarishwa katika maeneo yaliyoathirika.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime