Miaka kumi ya Jembefm

Kwa heshima na upendo mkubwa, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wasikilizaji wetu wote wa Jembe FM kwa kutembea nasi katika safari ya miaka 10 hakika mmetupa nguvu, hamasa na sababu ya kuendelea kufanya kile tunachokipenda kila siku bila nyinyi, Jembe FM isingekuwa mahali hapa ilipo leo.

Tumejifunza, tumekua, tumecheka na hata kutafakari pamoja—kila siku ikawa ni safari mpya yenye thamani kwa sababu ya uwepo wenu ,  upendo, maoni, uaminifu na muda wenu ni zawadi kubwa kwetu. Kwa kweli, mmekuwa zaidi ya wasikilizaji; mmekuwa marafiki, ndugu na kiungo muhimu cha familia yetu.

Tunawashukuru sana kwa kutupa time, kwa kuwa sehemu ya #FamiliaMoja yenye mvuto wa kipekee. Miaka 10 ni mwanzo tu—tunaamini mbele kuna mengi zaidi ya kuijenga, kuiboresha na kuifurahia pamoja. Asante kwa kila hatua, kila sikio na kila moyo uliojitoa kutusikiliza. Jembe FM inasema: #Ahsante kwa time # familia moja 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii