Mahakama yamhukumu Nzumbi Magumba mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa kijiji cha Lali kilichopo wilaya ya Itilima mkoani Simiyu kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka mtoto wa mke wake.
Magumba ameshitakiwa kwa kosa moja la kubaka kinyume na kifungu cha 130(1)(2)(e) na 131(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 202.
Awali mahakamani hapo imedaiwa na mwendesha mashtaka mkaguzi kutoka jeshi la polisi Jaston Mhule kuwa Agosti 24 mwaka huu katika kijiji cha Lali wilayani Itilima mzazi wa mhanga alibaini mtoto wake mwenye umri wa miaka 10 jina linahifadhiwa amebakwa na baba yake mlezi baada ya yeye kurudi kutoka safari na taarifa zilifika kituo cha polisi na mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi wilayani hapa kwa mahojiano baada ya upelelezi kukamilika ilibainika kuwa mshtakiwa alikuwa akimbaka mhanga nyakati za usiku kwa siku ambazo mke wake alikuwa amesafiri.