Kilio katika msiba ni tukio la kawaida duniani Kote,.
Nisauti ya huzuni,upendo na hisia ambazo maranyingi maneno hushindwa kueleza.
Watu hulia si kwasababu ni dhaifu ,bali kwasababu mioyo yao imeguswa na tukio la kuondokewa na mpendwa .
Lakini je,kilio hiki ni utamaduni,ni maandiko ya Biblia ,au ni hali ya kisaikolojia ya mwanadamu?
Kilio kama tiba ya moyo: Kwamujibu wa wataalamu wa kisaikolojoa,kulia ninjia ya mwili kujibu maumivu ya kihisia.
Machozi huondoa kemikali za msongo wa mawazo (Stress) na hivyo kumpa mtu utulivu wa ndani.
Kilio husaidia kutuliza huzuni ,kama mlango wa kutolea maumivu ya moyo .
Kwa lugha rahisi Tunalia ili tuweze kupona" Kilio ni tiba ya moyo uliojeruhiwa".
Maana ya tamaduni: Katika utamaduni nyingi za kiafrika,kulia msibani ni ishara ya upendo na heshima .
Watu hulia ili kuonyesha mshikamano na familia ya marehemu ,kwa jamii nyingi,mtu ambaye halii msibani huonekana kama asiye na hisia ,au mwenye ukatili wa moyo.
Kuna hata mila ambazo hulazimisha maombolezo ya pamoja,yakionyesha kwamba kifo si cha familia moja bali cha jamii nzima.
Uhalali wa kilio katika Biblia : Biblia yenyewe haikatazi kulia ,Yesu Kristo mwenyewe alilia alipomwona rafiki yake Lazaro amekufa( Yohana: 11: 35"Yesu akalia").
Viongozi wa Israel pia walilia walipopoteza wapendwa wao kama Musa na Yakobo.
Hivyo kilio kinatambulika kama ishara ya upendo ,maombolezo ,na unyenyekevu mbele za Mungu.
Ni sehemu ya imani kwamba kwa kupitia machozi moyo unamkabidhi Mungu maumivu yake.
Kwanini Marehemu husifiwa zaidi baada ya kufa? Ni jambo la kawaida sifa kedekede baada ya mtu kufariki.
Maneno ambayo pengine haya kuwahi kusemwa akiwa hai.
Sababu kuu ni hisia za majuto: kifo huwa kama kioo kinachotuonyesha thamani ya mtu aliyepotea.
Wengine husema mazuri kama njia ya kuleta faraja kwa familia ,au kutokana na imani kwamba si vema kumzungumzia vibaya marehemu.
Hata hivyo,Swali lina baki ; Je,ni sawa tusubiri mtu afe ndipo tumsifu? Jibu ni hapana.
Ni vizuri kumwambia mtu uzuri wake akiwahai,kwani baada ya kufa,hana masikio ya kusikia.
" Niheri kumpa mtu maua yake akiwa hai, kuliko shada kaburini".
Kilio ni sauti ya upendo ,na sifa ni alama ya heshima.
Lakini tusisubiri majonzi ndipo tuonyeshe upendo.
Tutawathamini wazazi ,marafiki na ndugu zetu sasa wakati bado tuko nao.
kifo ni mwalimu wa ukimya ,lakini upendo wa kweli ni tendo la sasa.(Makala hii nijibu la msomaji wangu aliyependa kujua kwanini marehemu hupata sifa nyingi,tofauti na kipindi cha uhai wake.).