Mamba ni wanyamapori hodari sana katika masuala ya kuvizia, kuvumilia na kufanya mashambulio ya kushtukiza. Mara zote hukaa kimya kabisa wakiwa wamechutama ndani ya maji kiasi kwamba macho na pua pekee wakati mwingine yakitokeza juu ya uso wa maji au huzama kabisa asionekane.
Uvumilivu wao ni wa kipekee kwani wanauwezo wa kusubiri kwa masaa kadhaa, siku au wiki nzima wakisubiria mawindo yao yasogelee lile eneo maalum walilolikusudia.
Wanyamapori hawa wamejariwa kuwa na vipokea mitetemo ya mawimbi (Vibration Sensors) zilizopo chini ya mataya yao pindi mnyama anayemuwinda anapokanyaga maji, uwezo wa kuhisi mitetemo hiyo ni kuanzia umbali wa mita 10 hadi 20 akiwa amezama ndani ya maji.
Pindi mnyama anapokaribia bila wasiwasi, mamba hufyatuka kwa kasi ya ajabu mithili ya muungurumo wa radi, akitumia mkia na miguu yake ya nyuma yenye nguvu kufanya shambulio la kushtukiza (surprise attack).
Makamanda wanajua maana halisi na mafanikio lukuki ya “surprise attack” ila kwa faida ya wasomaji wangu zaidi ya asilimia 90 ya shambulio la aina hii huwa na matokeo chanya.
Kwa historia kemkem ya mamba na viumbe hai waotegemea maji kuendesha maisha yao; *Hifadhi ya Taifa Rubondo* ndilo jibu lako.