Wakazi wa Shinyanga watakiwa kujitokeza katika kambi ya Madaktari Bingwa

Kambi ya Madaktari Bingwa wa Mama Samia ni mpango wa serikali ya awamu ya tano ya kusogeza huduma za afya kwa wananchi hasa huduma za kibingwa, na kupunguza adha inayosababishwa na ufinyu wa hospitali kuu mikoani.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amewaomba wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi ili kupata uchunguzi na ushauri wa matibabu ya kibingwa kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Mama Samia waliopiga kambi ya siku tano mkoani humo.

Mhita ametoa wito huo leo Oktoba 13 mwaka huu wakati akiwapokea Madaktari Bingwa 36 walioMkuu huyo wa mkoa amesema madaktari hao wamekusudiwa kusogeza huduma za afya za kibingwa karibu na wananchi na itakuwa  fursa muhimu kwa wakazi kupata huduma za afya bila usumbufu wa usafiri au gharama kubwa.

Aidha Mhita ameongeza kuwa hii ni awamu ya nne ya kambi ya Madaktari Bingwa kufanyika mkoani Shinyanga ambapo hadi sasa kambi hizo zimehudumia zaidi ya wananchi 240,000 na kujengea uwezo wataalamu 15,000 wa halmashauri za mkoa.

Kwa upande wake Mratibu wa Kambi Michael Mbele amesema wamejipanga vizuri kutoa huduma bora kwa wananchi na wanatarajia kuwafikia zaidi ya watu 30,000 katika kipindi cha siku tano cha kambi hiyo.wasili Shinyanga ambao wamegawanywa katika halmashauri zote sita za mkoa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii