RAPA mkongwe kutoka Nchini Marekani ameweka wazi
kuwa licha ya kwamba hayuko sana katika soko la muziki wa Hip Hop na Filamu
kama ilivyokuwa mwanzo, Biashara yake ya Dawa za Kuongeza nguvu za kiume
imemlipa kwa kiwango kikubwa tofauti na alivyotegemea.
Akifunguka katika moja ya interview hivi karibuni,
Camron amesema kwamba Bidhaa yake hiyo ya kuongeza nguvu za kiume ambayo
inafahamika kwa jina la PINK POWER HORSE,
imemlipa kiasi cha USD Milioni 10 (Sawa
na Tshs 24,527,213,400) ndani ya Miaka
Minne.
Pia Camron amesema Mzigo huo ni asilia na
Malighafi zake huwa anazitoa Nchini Senegal, ambapo huwa ni Mizizi ya Miti,
Majani ya Miti, hivyo tangu ameanza biashara hiyo mpaka hivi sasa imempatia
manufaa makubwa sana.