FAT JOE: Bruno Mars Alinifokea Baada Ya Kumuuliza Asili Yake Kama Ni Puerto Rico

Rapa Fat Joe amefunguka namna ambavyo ailumizwa moyo na majibu ya msanii mwenzake Bruno Mars baada ya "kumchenjia" mbele za watu pasipo kuangalia njia sahihi ya kumjibu baada ya kumuuliza kama yeye ana asili ya Puerto Rico.

Akizungumza katika Podcast yake ya JOE & JADA, Fat Joe amesema kuwa, yeye amekuwa ni shabiki mkubwa sana wa Bruno Mars kwa muda, lakini Tukio hilo lililotokea mika 10 mpaka 15 iliyopita katika moja ya tuzo, lilimvunja moyo sana

Joe anasimulia kuwa, alikuwa ni mtu ambaye alitamani sana kuonana Bruno Mars baada ya kusikia kuwa yeye asili yake ni Puerto Rico, na siku hiyo alikuwa amekaa pembeni yake. Wakati anajiandaa kuongea naye, kuna mtu mwingine pembeni alimuonya Fat Joe kuwa asimuongeleshe Bruno Mars suala hilo, maana ni Mtata kweli kweli, Lakini Fat Joe akaona haina ishu , ngoja amuulize

Katika hali ya Uchangamfu, Fat Joe alimuita Bruno Mars na kumwambia “Yo Bruno Niaje”, na Bruno akamjibu Fat Joe kuwa “Mambo Vipi Joe?”. Fat Joe akamuuliza Bruno “Oya, Wewe una Asili ya Puerto Rico?” lakini Bruno alimjibu “Unazungumza Upuuzi Gani?, Mimi ni Raia Wa Puerto Rico?, usithubutu kuniuliza tena swali la kipuuzi kama hilo maishani Mwako”

Fat Joe anaongeza kuwa , Kauli hiyo ilimuuma na kumvunja moyo sana maana alipayuka kwa nguvu sana

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii