WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Oktoba 16 mwaka huu ni mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Tanga kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Usagara.
Madhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka yanalenga kuamsha ari ya uzalishaji wa mazao ya chakula ikiwemo yaliyoongezewa virutubishi; kuhimiza ulaji bora na kuongeza tija ya uzalishaji wa chakula ili kujihakikishia usalama wa chakula na lishe kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.
Maadhimisho hayo yanakaulimbiu isemayo “Tuungane Pamoja Kupata Chakula Bora Kwa Maisha Bora Ya Baadaye.”