Hizi ndizo familia maarufu za kihalifu (mafia) zilizoanza zamani lakini bado zinahusishwa na shughuli haramu hadi leo kimya kimya:
1. Familia ya Gambino – New York
Iliongozwa na nguli John Gotti “The Dapper Don”, lakini pichani ni Paul Castellano – aliyefahamika kama The White Collar Don, na hata kuimbwa na Mh. Hamis Mwinjuma (Mwana FA): ‘’The White Collar Don Kama Paul Kama Paul Castellano…”
- Alipigwa risasi 6 mwaka 1985.
- Utajiri wao: Zaidi ya Tsh Trilioni 7
- Wanachama: Zaidi ya 2,000
2. Familia ya Genovese – New York
Kama ulishasikia Billnass akisema “MAFIOSO” basi ndiyo huyu Vito Genovese kwani ni Mafia haswa, kiongozi wa Kundi la Genovese ambaye kwenye kulinda maslai ya biashara zake haramu aliwahi kumuunga mkono Benito Mussolini kwenye WWII (1937).
- Ushawishi wao si NewYork pekee bali ni kwenye majimbo zaidi ya 7
- Wanachama: Zaidi ya 2,500
- Utajiri: Zaidi ya Tsh Trilioni 9
3. Chicago Outfit – Chicago
Ilipata umaarufu mkubwa chini ya Al Capone (Pichani) mwaka 1925 na ukisikia watu wanatumia jina ‘’Notorious’’ Biggie na wenzake basi huyu ndiyo mkubwa wa kazi mwenyewe sasa. Chicago Outfit siyo sehemu ya “Five Families” za New York, lakini ina nguvu kubwa katika maeneo ya Midwest.
NB: Haya makundi yote ya Mafia hayana ukubwa sana na umaarufu kama zamani na hii ni kutokana na mashinikizo ya FBI na mabadiliko ya karne, lakini bado wapo.