Sudan Kusini kuwarejesha wahamiaji nchini mwao

 SERIKALI ya Sudan Kusini imesema ipo katika mazungumzo na baadhi ya nchi za kigeni ili kuwarejesha wahamiaji waliopokelewa kutoka Marekani mwezi Julai mwaka huu. Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Apuk Ayuel Mayen, mazungumzo hayo yanalenga kuhakikisha wahamiaji hao wanarejeshwa katika mataifa yao ya asili.

Sudan Kusini iliwapokea wahamiaji wanane waliorejeshwa kutoka Marekani chini ya mpango wa Rais wa Marekani, Donald Trump, wa kuondoa wahamiaji wasio na vibali nchini humo. Hata hivyo, kati ya wahamiaji hao wanane, mmoja alibainika kuwa raia wa Sudan Kusini, huku wengine wakitambulika kutokea mataifa mengine.

Kwa mujibu wa taarifa, wahamiaji hao walikuwa wamehukumiwa kwa makosa makubwa ya jinai kabla ya kurejeshwa. Trump, aliweka msisitizo mkubwa kwenye sera ya kuwarejesha wahamiaji wasio na vibali katika nchi walikotokea au katika mataifa maskini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii