Kardinali Protase Rugambwa akutana na Samia Tabora

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Kardinali Protase Rugambwa pamoja na Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo hilo Mhashamu Baba Askofu Paul Ruzoka Ikulu Ndogo ya Tabora leo Septemba 12 mwaka huu. 

Pamoja na mambo mengine Maaskofu hao walimuombea Rais Dkt. Samia ambaye anagombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

 Pichani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Kardinali Protase Rugambwa pamoja na Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo hilo Mhashamu Baba Askofu Paul Ruzoka mara baada ya kuwasili Ikulu Ndogo ya Tabora Septemba 12 mwaka huu. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii