Mgombea urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Gombo Samandito Gombo amevitaka vyombo vya dola Nchini kutenda haki kwa vyama vyote vya siasa kwakuwa vipo kwajili ya kuwahudumia watanzania wote.
Kauli hiyo ameitoa kwenye mkutano wa hadhara iliofanyika Kata ya Mahembe Jimbo la Kigoma Kaskazini Mkoani Kigoma ambapo amevitaka vyombo vya dola kutotumika vibaya.
"Vyombo vya dola visitumike vibaya na ccm nyinyi ni wa wote hakikisheni kila mtanzania yupo salama mkilalia upande mmoja madhara yakitokea hakuna atakayebaki salama, "alisema Gombo.
"Hata nyinyi wenyewe mna watoto mna wazazi wenu huko waliko likirindima tu jambo hapa wewe kaa ni askari uko Kigoma na wewe nyumbani kwenu ni Mwanza shughuli itakayofanyika kwanza hutokuwepo wewe watafanyiwa wao kwahiyo vyombo vya dola niviombe vizingatie haki za watanzania vyombo vya dola ni mali ya watanzania wote ni lazima vitende haki, "amesisitiza Gombo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mipango na uchaguzi CUF Yusuf Mbungilo amesisitiza vyombo vya dola kuzingatia sheria za mikutano ya vyama husika katika maeneo vilivyopangiwa.