MASHINDANO YA THE ANGELINE CUP YAZINDULIWA ILEMELA

Mashindano ya The Angeline Cup yamezinduliwa rasmi kwa msimu huu katika Jimbo la Ilemela, mkoani Mwanza, yakibeba kauli mbiu isemayo “Shiriki Uchaguzi kwa Maendeleo Yako.”

Mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kwa zaidi ya miaka tisa sasa, yameendelea kuwa chachu ya mshikamano na maendeleo ya jamii ya Ilemela.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ndiye muasisi wa mashindano hayo, Angeline Mabula, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Bi. Mabula amesema ni haki ya kila Mtanzania kuhakikisha anajitokeza siku hiyo muhimu ya kupiga kura, na akawataka wananchi kumchagua Rais Samia Suluhu Hassan ili kuendeleza kasi ya maendeleo nchini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii