Zanzibar yatoa ratiba ya kura za mapema Oktoba 28

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na Madiwani.

Akizungumza leo Agosti 18, Mwenyekiti wa ZEC Jaji George J. Kazi amesema kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 34(3) na (4) cha sheria ya uchaguzi na. 4 ya mwaka 2018 Uchaguzi Mkuu utafanyika Jumatano ya October 29 mwakahuu.

Aidha, kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na. 4/2018, kutakuwa na upigaji kura za mapema utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya kura za pamoja ambazo kikawaida huhusisha Wananchi wote.

Kura za mapema zitazopigwa October 28 zitawahusisha Watendaji na Askari wanaosimamia shughuli za uchaguzi wakiwemo Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasaidizi, Wasimamizi wa Vituo, Askari Polisi watakaokuwa kazini, Wajumbe wa Tume pamoja na Watendaji wa Tume ya Uchaguzi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii