Kesi ya Lissu yaendelea leo mahakamani

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu inatarajiwa kusikilizwa leo katika Мahakama уа Hakimu Mkazi Kisutu, huku ikiwa imepanga kutoa amri kuhusu kurushwa mubashara kwa maelezo ya mashahidi katika kesi hiyo.

Pia Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga anayesikiliza kesi hiyo kwa alisema, leo Agosti 18 mwaka huu upande wa Jamhuri utamsomea mshtakiwa Lissu maelezo ya kesi ((Commital) ili kesi iweze kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Hatua hiyo inakuja kufuatia uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu wa kubariki mashahidi ambao ni raia katika kesi hiyo kufichwa ili kulinda usalama wao.

Itakumbukwa kuwa Agosti 13,2025 Wakili wa serikali Mkuu Nassoro Katuga aliikumbusha mahakama juu ya uamuzi wa mahakama kuu uliotolewa Agosti 4, ambao ulitoa amri mbali mbali sita ikiwemo vyombo vya habari kutoruhusiwa kutangaza mubashara taarifa za mashahidi ambao ni raia (commital) na ushahidi wakati wa usikilizwaji wa kesi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii