Waziri wa Utamaduni Sanaa na
Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa leo Februari 13, 2022 anatarajia
kushiriki kwenye kilele cha Tamasha la kimataifa la Sauti za Busara la
mwaka huu Zanzibar.
Tamasha la Sauti za Busara ni miongoni mwa
matamasha makubwa nchini ambayo yamefanikiwa kuonesha utamaduni wa nchi
Tanzania duniani kupitia Sanaa za muziki.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi ambaye anashiriki
amesema tamasha la mwaka huu limeboreshwa zaidi ukilinganisha na miaka
ya nyuma.
Aidha, amesema kutokana na tamasha hili amejifunza
mengi ambayo yanaweza kusaidia kuboresha matamasha yanayokwenda
kuandaliwa hivi karibuni.
“Tumejifunza mengi katika tamasha hili,
tutatumia, kazi iliyombele yetu ni kubeba mambo mazuri ya tamasha hili
kuboresha matamasha yanakuja mbele yetu yawe kwenye hadhi ya kimataifa
ili kuitangaza Tanzania na kuuza utamaduni wetu duniani kama tulivyo
elekezwa na Rais wetu kipenzi, Mhe. Samia Suluhu Hassan”. Ameongeza Dk.
Abbasi
Pia katika tamasha hili Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma ameshiriki.
Awali
Rais Samia katika tamasha la utamaduni la mkoa wa Kilimanjaro
alielekeza Wizara ya utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na wadau
kuandaa matamasha makubwa ambayo yatasaidia kutangaza utalii na
utamaduni wa Taifa la Tanzania kimataifa.
Hivi karibuni Rais wa
Zanzibar. Mhe, Hussein Alli Mwinyi ameliezea Tamasha la Sauti za Busara
kuwa lina mchango muhimu wa kuhamasisha umoja na mshikamano nchini.