Mvua yasababisha maafa nchini Pakistan

SERIKALI ya Pakistan imeamuru kufungwa kwa biashara, shule na ofisi za umma mjini Karachi baada ya mvua kubwa kusababisha vifo vya watu 10.

Taarifa zinasema vifo hivyo vilitokana na kuzama majini, ajali za barabarani, kuanguka kwa majengo na kupigwa na umeme.

Mvua hiyo, iliyoanza Jumanne, imefikia viwango ambavyo havijashuhudiwa kwa miaka mingi katika maeneo ya kusini mwa mji huo wenye watu zaidi ya milioni 20.

Aidha, mafuriko yamesababisha madhara makubwa nchini kote huku idadi ya vifo katika eneo la milimani kaskazini magharibi ikifikia watu 385 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii