Moto umezuka na kuteketeza nyumba yenye vyumba tisa ambayo anaishi mmoja kati ya wachungaji wa iliyotokea usiku wa Agosti 20 mwaka huu hakuna mtu aliyepoteza maisha lakini mali mbalimbali zilizokuwamo zimeteketea.
Mchungaji Amosi Chidemi ambaye alikuwa anaishi katika nyumba hiyo amesema saa moja usiku wakati akiwa sebuleni na familia yake wakaona moshi unajaa ndani na baada ya kwenda kuangalia unapotokea moshi wakaona moto tayari umeshatanda katika baadhi ya vyumba.
Amesema yeye pamoja na familia yake wametoka salama lakini hajui nini ambacho kimeokolewa mpaka kwani majirani walianza uokoaji wakati tayari moto umeshakuwa mkubwa.
“Wakati tumekaa sebuleni, tumemaliza kula chakula tukawa tunaongea, tukashangaa moshi unaingia sebuleni.
Nikatoka ili niangalie moshi unatoka wapi ndio nikakuta ile pazia ya kwenye korido ndio imeshatanda moto ukiwa ni mkali kabisa, mke wangu akanivuta kwamba tutoke nje kupitia mlango mwingine, ndio tukanusurika wote," amesema.