Afghanistan 79 wafariki kwa ajali wakitokea Iran

Watu 79 wakiwemo watoto 19, wamefariki dunia baada kutokea ajali ya basi  katika Jimbo la Herat kaskazini magharibi mwa Afghanistan ikihusisha  lori pamoja na pikipiki.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa wizara ya  Mambo ya Ndani nchini humo, Abduli Qani imesema ajali hiyo imesababishwa na basi walililokuwa wakisafiria watu hao kugongana na lori na pikipiki wakiwa njiani kurejea nchini humo wakitokea Iran.

Imeelezwa watu hao walikuwa wanarejea nchini humo baada ya kufukuzwa katika maeneo waliokuwa wamehifadhiwa Iran.

Amesema kuwa jumla ya waliofariki kwenye ajali hiyo ni  79 wakiwemo watoto 19 huku watu wawili walijeruhiwa.

Daktari mkuu wa hospitali ya kijeshi, Mohammad Janan Moqadas amesema miili mingi imeshindikana kutambulika kwasababu imeungua.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii