Rais Mwinyi awasili Dodoma vikao vya uteuzi Wagombea

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili jijini Dodoma kushiriki katika vikao vya kikatiba vya Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Taifa.

Katika uwanja wa ndege wa Dodoma, Rais Dkt.Mwinyi amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule na viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CCM, ajenda kuu ya vikao hivyo vinavyotarajia kuanza kesho Agosti 21 ni uteuzi wa wagombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Viti Maalum, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii