Zaidi ya wananchi 10,000 kupatiwa miwani ya macho bure

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Charles Mkombachepa amesema zaidi ya wananchi 10,000 watapatiwa bure miwani za macho wakati wa Tamasha la Tanzania Samia Connect litakalofanyika Agosti 21 hadi 23, kwenye Viwanja vya Mgambo, Jijini Arusha.


Amesema pamoja na huduma hiyo, wananchi watapimwa na kupewa ushauri kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu na saratani.

Tamasha hilo linaratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha chini ya Kenani Kihongosi na litahusisha pia huduma bure za vyeti vya kuzaliwa, vitambulisho vya taifa, hati za ardhi, elimu ya mikopo, pamoja na burudani mbalimbali.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii