Kiongozi wa Upinzani wa chama cha NUP nchini Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu, almaarufu Bobi Wine, amethibitisha nia yake ya kuwania urais wa Uganda katika uchaguzi mkuu wa 2026 baada ya chama chake kuchukua fomu za uteuzi kutoka Tume ya Uchaguzi mjini Kampala.
Hili litakuwa jaribio lake la pili la kutafuta urais wa Uganda, miaka mitano baada ya kushindwa uchaguzi wa 2021 na Rais Yoweri Kaguta Museveni.
Jumatatu, Bobi Wine aliwakilishwa katika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Joel Ssenyonyi, pamoja na Katibu Mkuu wa NUP David Lewis Rubongoya na viongozi wengine wakuu wa NUP.