Agosti 18 mwaka huu Mamlaka ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ilimshikilia anayedaiwa kuwa 'daktari feki', akifahamika kwa jina la Mussa, baada ya kugundulika na baadhi ya Wagonjwa kutaka kuwatapeli, alipohojiwa alikiri hana Elimu ya taaluma hiyo na kukana madai hayo ya kutapeli Wagonjwa.
Taarifa ya Mganga Mkuu Mfawidhi wa Amana, Dkt. Bryceson Kiwelu imeeleza kuwa Mtuhumiwa alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi huku Wagonjwa kadhaa wakikiri kuwa walikuwa mbioni kutapeliwa na Mtu huyo kabla ya kukamatwa.
Aidha, Mussa aliwahi kukamatwa mnamo Agosti 30, 2023, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akihusishwa na matukio ya utapeli kwa Wagonjwa ambapo alikiri kuwa ni kweli alikuwa hospitalini hapo kufanya utapeli.