Bot yauawa takribani watu 68

Takribani wahamiaji 68 wamefariki dunia baada ya boti iliyokuwa imebeba takriban watu 150 kuzama katika pwani ya Yemen kufuatia hali mbaya ya hewa mnamo Agosti 3 mwaka huu 

Chombo hicho kilizama katika jimbo la kusini mwa Yemen la Abyan, na miili 68 imepatikana, huku watu 12 wakiokolewa wakati wengine 74 wakiwa bado hawajapatikana.

Wengi wa waathiiriwa wanaaminika kuwa raia wa Ethiopiakwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji nchini Yemen (IOM), ambalo limelitaja tukio hilo kuwa la kuhuzunisha.

Yemen inasalia kuwa njia kuu ya wahamiaji kutoka Pembe ya Afrika wanaosafiri kwenda mataifa ya Ghuba ya Kiarabu kutafuta kazi, huku IOM ikikadiria kuwa mamia wamekufa au kupotea katika ajali kama hizo katika miezi ya hivi karibuni.

Yemen ni nchi maarufu ambapo wahamiaji wengi waliokata tamaa wanaoelekea kaskazini mwa Saudi Arabia hupita ili kwenda kutafuta fursa bora zaidi za maisha. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii