Mtu mmoja Mkazi wa Mtaa wa Kusenha Kata ya Matumbulu jijini Dodoma ajulikanaye kama Frank Sanga (33) ameuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi kutokana na mvutano uliotokea kati ya askari hao na wananchi mara baada ya kumkamata dereva wa pikipiki aliyekuwa amebeba magunia ya mkaa.
Ni simanzi na majonzi kwa familia ya marehemu Sanga ambao mpaka hivi sasa wamekataa kuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi wakitaka kujua hatua za kisheria dhidi ya askari polisi waliohusika na Tukio hilo.
David Sanga ni ndugu wa marehemu na mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo hapa anaeleza alivyoshuhudia ndugu yake akipoteza maisha.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo, Noah Zakayo ameliomba jeshi la polisi kuwachukulia hatua kali za kisheria askali polisi waliotekeleza mauwaji hayo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma Gallus Hyera amesema wanawashikilia askari polisi hao huku akielezea sababu za chanzo cha kifo cha Frank.