Msanii wa Muziki wa
Kizazi kipya nchini Kenya, Colonel Mustapha ameweka wazi kuwa moja kati ya vitu
ambavyo anavijutia mpaka hivi sasa, ni kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
wasanii maarufu nchini humo.
Akizungumza katika
mahojiano nchini humo, Colonel ambaye alifanya vema na nyimbo tofauti kama vile
MTAANI.COM amesema kuwa hivi sasa yupo katika mahusiano mapya na binti mwingine
ambaye hana umaarufu wowote ule na ana ulemavu wa kusikia yaani “Kiziwi”, na
hatamani hata kidogo kuwa na mahusiano na mtu maarufu.
Msanii huyo ameongeza
kuwa, kuwa na mahusiano na wasanii maarufu ni “Pasua Kichwa” na huwa na
usumbufu mkubwa kitu ambacho kimemrudisha nyuma kimaendeleo japo hivi sasa
ameanza kurudi katika ubora wake hasa kiuchumi.
Pia amebainisha kuwa,
mpenzi wake wa sasa ambaye ni Kiziwi watu wengi hawamfahamu kwa sababu hajamuanika
mitandaoni, ila muda ukiwadia atafanya hivyo.
Kwa mujibu wa maelezo
yake, mpenzi wake huyo alipata ulemavu wa kutokusikia kutokana na ajali ya gari
aliyopiata akiwa katika umri mkubwa, ajali iliyopelekea kupondwa na jiwe
kichwani na kupata changamoto hiyo