Waziri Mkuu aendelea na ziara yake nchini Belarus

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Julai 21, 2025 aliwasili nchini Belarus kwaajili kuanza ziara yake ya kikazi nchini humo Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kinsk na kupokelewa na Naibu Waziri Mkuu wa Beralus, Viktor Karankevich. 

Katika ziara hiyo siku ya Kwanza Mheshimiwa Waziri Mkuu aliweka shada la maua katika mnara wa mashujaa wa Jamhuri ya Beralus.

Pia atatembelea kiwanda cha kutengeneza Matrekta na vifaa mbalimbali vya kilimo (Minsk Tractor Plant) na baadae atakutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Belarus Mhe. Alexander Turchin.

Katika ziara hiyo ameambatana na Balozi wa Tanzania Urusi na Belarusi, Frederick Ibrahim Kibuta , Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Kazi , Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Shariff Ali Shariff na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii