Akutwa amefariki akiwa chumbani kwake

Mwili wa aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kageme Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga  Juliana Mkumbo (30) amekutwa amefariki dunia ndani ya chumba chake,baada ya kutoonekana kwa muda mrefu huku uchunguzi wa awali wa kitabibu ukionesha alikunywa sumu ya Panya.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi amesema baada jeshi la  Polisi kupata taarifa za tukio hilo walifika na kuuchukua mwili huo kwaajili ya uchunguzi wa Kitabibu na Madaktari wamebaini Marehemu kunywa sumu ya panya.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii