Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole @hpolepole ametoa wito kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi @ccmtanzania kutokukalia kimya matukio ya aina yoyote ya uvunjifu wa haki za wengine kwani yatahatarisha amani na kupunguza imani ya chama hicho kwa wananchi.
Polepole ameyasema hayo leo Julai 18, 2025 katika mkutano wake anaoufanya na waandishi wa habari kwa kutumia mitandao.
“kuhusu haki kwanza CCM msione aibu kuzungumza kuhusu haki huwezi kupata amani bila haki, inaanza haki halafu inakuja amani na msingi wa uongozi wa CCM ni kuheshimika watu na haki” amesema Polepole
Hata hivyo ameongeza akisema “haki ni muhimu haki za watu wetu na haipendezi kuona watu wanapokwa haki zao na chama kimekaa kimya haikubaliki kabisa”