Ahukumiwa miaka 60 kwa kulawiti

Mahakama ya wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga  imemuhukumu Saidi Omary Mtangi mkazi wa Maramba wilaya ya Mkinga kifungo cha miaka 60 jela mara baada ya kukutwa na hatia ya kubaka na kulawiti watoto wawili kwa nyakati tofauti.

Mahakama imetoa adhabu ya miaka 30 kwa kila kosa moja ambapo adhabu hiyo  itatekelezwa mfululizo, hivyo kufanya kifungo kuwa jumla ya miaka 60.

Hakimu Mfawidhi, Mheshimiwa H.L. Rutehangwa, amesema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ulikuwa wa kuaminika na haukuwa na mashaka yoyote.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii